Chifu ahukumiwa 10 gerezani kwa kucharaza hadi kufariki watoto wawili
Chifu Msaidizi Stephen Kinyua/Hisani

Chifu ahukumiwa 10 gerezani kwa kucharaza hadi kufariki watoto wawili

Wavulana hao walituhumiwa kuiba Sh16,000 za muuza maji.

Chifu mmoja amehukumiwa miaka 10 gerezani kwa kusababisha mauaji ya watoto wawili katika kisa cha kusikitisha kilichotokea Novemba 30, 2012.

Watoto hao wawili, Alex Munene na Godfrey Mutuma, ambao wakati huo walikuwa na umri wa miaka 9, walikumbana na mauti yao baada ya kuteka maji katika kjiji jirani na mwanzao kwa jina Jones Mutethia, aliyenusurika na majeraha makubwa.

Mutethia anasimulia kuwa walivamiwa na watu watano katika nyumba zao mwendo wa saa tatu usiku wakiwatuhumu kumuibia muuzaji maji kwa jina Rahab Kananu KSh16,000.

Babake Mutuma, Peter Kailemia, alijitolea kuuza ng’ombe wake ili kulipa deni hilo lakini walikataa na kuripoti kwa chifu msaidizi Stephen Kinyua.

Chifu huyo aliamuru wavulana hao kutandikwa hadi kufichua aliyeiba pesa hizo.

Wavulana hao walibururwa hadi msituni wakitandikwa na kiboko chenye miba kwa muda wa saa mbili na kupelekea kifo cha wawili hao huku rafiki yao akiachwa na majeraha makali.

Kinyua alikamatwa siku iliyofuata na kushtakiwa kwa mauaji ya watoto hao wawili.

Baada ya muda mrefu wa kusaka haki, familia ya vijana hao watatu sasa imeridhika baada ya Jaji Thripsisa Cherere wa Makama Kuu ya Meru kumhukumu Kinyua mnamo Machi 2023 miaka 10 jela mnamo Aprili 30, akinyimwa kifungo cha nyumbani.

Share this article
Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *