Magazetini: Magavana 30 waunga mkono urais wa Raila

Magazetini: Magavana 30 waunga mkono urais wa Raila

Magazeti ya Jumanne, Januari 18, yameangazia uchaguzi mkuu wa Agosti 9 huku magavana 30 wakimuunga mkono kinara wa Orange Democratic Movement (ODM), Raila Odinga kuingia Ikulu.

Daily Nation

Raila amepigwa jeki na magavana wapatao 30 katika azma yake ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu.

Hatua hiyo inamuweka waziri huyo wa zamani katika nafasi nzuri ya kuzoa kura nyingi za maeneo na vilevile uwezo wa kifedha wa kufadhili kampeni za kitaifa.

Raila aliidhinishwa na magavana hao wakati wa mkutano mjini Naivasha mnamo Jumatatu, Januari 17.

Wakati wa hafla hiyo, gavana wa Makueni, Kivutha Kibwana, alifuta azma yake ya kuwania urais ili kumuunga mkono Raila.

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *