Mwanamume wa miaka 30, mkaazi wa Eldoret, ameshtakiwa kwa tuhuma za kuishi na msichana wa miaka 15 kwa zaidi ya miezi 10 kinyume cha sheria na kisha kumnajisi na kumpachika ujauzito.
Mshukiwa, Douglas Kagai, mlinzi wa kibinafsi, inasemekana alitekeleza unyama huo kati ya Aprili 8, 2019 na Februari 29, 2020.
Kagai alishtakiwa katika mahakama ya Eldoret ambapo mwathiriwa alisema Kagai alijidai kuwa afisa wa polisi ambaye angemsaidia kupata ajira katika kituo cha polisi cha Eldoret.
Inasemekana msichana huyo alikuwa ametoroka nyumbani kwao kutokana na dhuluma za kifamilia na alikuwa akiishi kaika kanisa moja kabla ya kukutana na Kagai.
Ad
Inasemekana mshukiwa alimfungia msichana huyo katika chumba chake kilichoko Kamukunji Estate, Eldoret, kila siku alipoondoka kwenda kazini. Alimruhusu tu kutoka nje asubuhi mapema na usiku ili asigunduliwe na majirani kabla ya kuokolewa na mzee wa kijiji ambaye alidokezewa na majirani
Kagai alipinga mashtaka hayo mbele ya hakimu mkuu wa korti ya Eldoret Richard Odenyo.
Kwa sasa amezuiliwa Eldoret baada ya kushindwa kulipa bondi huku mwathiriwa akipelekwa katika kituo cha watoto cha Huruma Children’s Rescue Centre mjini Eldoret.
Kesi hiyo itaendelea tena mnamo Mei 18, 2022.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.