Magazetini: Uhuru kukutana na viongozi wa Mulembe

Magazetini: Uhuru kukutana na viongozi wa Mulembe

Magazeti ya Jumanne, Januari 25, yanaripoti kuwa Rais Uhuru Kenyatta amewaalika wabunge kutoka jamii ya Luhya katika kile kinachoonekana kama njia ya kuzima ndoa ya DP William Ruto na kinara wa ANC, Musalia Mudavadi.

People Daily

Gazeti hili linaripoti kuwa Rais Uhuru hii leo Jumanne, Januari 25, atafanya mkutano na wabunge kutoka ngome ya Mudavadi baada ya kinara huyo wa ANC kuingia katika ndoa ya kisiasa na Ruto.

Baada ya mkutano huo, Uhuru pia atakutana na madiwani kutoka eneo hilo la Magharibi katika Ikulu, Nairobi, siku ya Jumatano, Januari 26.

Wabunge kadhaa wanaounga mkono Azimio la Umoja walithibitisha kupata mwaliko huo kupitia kwa Kiranja wa Bunge la Kitaifa ambaye pia ni Mbunge wa Navakholo, Emmanuel Wangwe.

Wengine walioalikwa ni maafisa wakuu serikalini wanaounga mkono handisheki akiwemo Waziri wa Ulinzi Eugene Wamalwa na viongozi wengine.

The Standard

Kulingana na gazeti hili, vuguvugu la Raila la Azimio La Umoja limewavuna viongozi wengi huku wanasiasa wakuu wa Murang’a wakitaka kutengewa nafasi ya mgombea mwenza.

Baadhi ya viongozi wa Murang’a ambao wanaunga mkono azma ya Raila kuwania urais ni ikiwemo mawaziri James Macharia (Uchukuzi), Irungu Wairagu (Maji) na seneta wa zamani Kembi Gitura.

Hata hivyo, wakati wa mkutano mtaani Thika Greens, eneobunge la Kandara siku ya Jumatatu, Januari 24, viongozi hao walimuomba Raila kumchagua mkaazi wa Murang’a kama mgombea mwenza wake.

Kiti hicho kimekuwa kikipigiwa upatu na Peter Kenneth na Waziri wa Kilimo Peter Munya.

Imehaririwa na Sam Oduor
Share this article
Show 1 Comment

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *