Magazetini: Raila awaonya wakenya dhidi ya DP Ruto, Mudavadi

Magazetini: Raila awaonya wakenya dhidi ya DP Ruto, Mudavadi

Magazeti ya Jumatatu, Januari 31, yameangazia siasa za humu nchini huku miungano kadhaa ikiendelea kubuniwa kuelekea chaguzi za Agosti 9.

Kinara wa ODM Raila Odinga amewaonya Wakenya dhidi ya kuwachagua vinara wa muungano wa Kenya Kwanza ambao unawaleta pamoja Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya, Moses Wetang’ula.

The Standard

Kinara wa ODM Raila Odinga amewaonya Wakenya dhidi ya kuwachagua vinara wa muungano wa Kenya Kwanza.

Muungano huo unawaleta pamoja Naibu Rais William Ruto, kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi na mwenzake wa Ford Kenya, Moses Wetang’ula.

Wakati wa ziara yake ya kampeni katika kaunti ya Nairobi siku ya Jumapili, Januari 30, Raila aliwarushia vijembe watatu akiwataja kama watu fisadi. Waziri mkuu huyo wa zamani alitaja kashfa kadhaa za ufisadi zinazowaandama vinara wa muungano huo.

Raila alitaja sakata ya KSh 280 milioni za makaburi ya Mavoko na KSh 4 bilioni za Anglo-Leasing na Goldenberg zilizomuhusisha Mudavadi, kuuzwa kwa ubalozi wa Tokyo nchini Japan ambapo Wetang’ula anatuhumiwa na sakata ya mahindi inayomuhusisha Ruto.

Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *