Magazetini: Aliyekuwa mkuu wa NSSF kulipa Sh 2.4b ama miaka 14 gerezani

Magazetini: Aliyekuwa mkuu wa NSSF kulipa Sh 2.4b ama miaka 14 gerezani

Magazeti ya Jumanne, Februari 1, yameipa uzito hukumu ya kihistoria katika kesi dhidi ya ufisadi baada ya waliolaghai Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii na Mafao (NSSF) kupigwa faini ya KSh 9.6 bilioni.

Magazeti haya pia yanaripoti kuwa kinara wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga amepigwa jeki baada ya vyama 13 vya kisiasa kukubali kumuunga mkono.

The Standard

Mnamo siku ya Jumatatu, Januari 31, mahakama moja iliweka rekodi baada ya kuwatoza washtakiwa wanne faini ya KSh 9.6 bilioni kwa kuibia NSSF KSh 1.2 bilioni.

Adhabu hiyo kali ilitolewa na Hakimu Mkuu Lawrence Mugambi kwa aliyekuwa meneja wa uwekezaji wa NSSF, Francis Moturi, na wakurugenzi wengine watatu wa kampuni ya kibinafsi

Moturi, David Githaiga, Wilfred Weru na Isaac Nyamongo ni lazima walipe faini hiyo ama wafungwe jela miaka 14.

Daily Nation

Vyama kadhaa vimekubali kuunga mkono vuguvugu la Raila la Azimio La Umoja.

Haya yanajiri wakati wiki hii mirengo ya kisiasa inazotazamiwa kutumika kwenye Uchaguzi Mkuu wa Agosti 9 kuanza kusajiliwa.

Kando na ODM na Jubilee kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta, vyama vingine vinavyounga mkono Azimio ni pamoja na kile cha Gavana wa Kitui, Charity Ngilu, National Alliance Coalition (Narc), cha gavana wa Machakos, Alfred Mutua Maendeleo Chap Chap (MCC), Ubuntu People’s Forum (UPF) kinachoongozwa na Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui.

Vingine ni kinachoongozwa na Gavana wa Pokot Magharibi, John Lonyangapuo, Kenya Union Party (KUP) na Pan African Alliance (PAA) cha Gavana wa Kilifi Amason Kingi.

Taifa Leo

Kulingana na gazeti hili, kivumbi kinatarajiwa katika kaunti tofauti nchini baada ya magavana wa zamani waliobwagwa katika chaguzi za 2017 kutangaza kurejea ulingoni.

Baada ya kuwa kwenye baridi kwa miaka mitano, magavana hao wanalenga kutumia miradi yao ya maendeleo walizoanzisha kujipigia debe.

Walipopoteza viti vyao, wengi wao walioteuliwa kuhudumu katika vyeo vya serikali pia wametazangaza azma yao ya kutetea viti vyao katika chaguzi za Agosti 9.

Magavana ambao wametangaza kurejea kutetea viti vyao ni ikiwemo Isaac Ruto (Bomet), Joshua Irungu (Laikipia), Ken Lusaka (Bungoma), na Moses Akaranga (Vihiga).

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *