Uhamisho: Aubameyang ahamia Barca kwa mkopo, Diaz aingia Liverpool kudumu
Pierre Emerick Aubameyang | Picha- Getty Images

Uhamisho: Aubameyang ahamia Barca kwa mkopo, Diaz aingia Liverpool kudumu

Dirisha la uhamisho barani Ulaya lilikamilika jana usiku huku baadhi ya timu zikifanyia mabadiliko vikosi vyao:

⦁ Everton, inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza, imekamilisha uhamisho wa kiungo wa kati wa Tottenham Hotspurs Dele Alli, mwenye umri wa miaka 25, kwa kandarasi ya kudumu. Timu hiyo pia imepata sahihi ya kiungo wa Manchester United na taifa la Uholanzi Donny de Beek kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu.

⦁ Liverpool wamepata sahihi ya Luiz Diaz kutoka AFC Porto kwa mkataba wa kudumu.

⦁ Newcastle imenasa beki wa Brighton Dan Burn, 29, kwa kitita cha million €15. Klabu hiyo pia imepata sahihi ya Bruno Guimarmaraers, 24, kutoka Lyon inayoshiriki ligi kuu ya Ufaranza.

⦁ Aliyekuwa kiungo wa timu ya taifa ya Uingereza na kocha wa Chelsea Frank Lampard ameteuliwa rasmi kuwa mkufunzi wa Everton. Lampard amekuwa bila klabu tangu atimuliwe Chelsea kutokana na matokeo duni.

⦁ Klabu ya Brentford imekamilisha uhamisho wa kiungo wa kati wa Denmark, Erickson, 29, kwa mkataba wa miezi sita.

⦁ Mshambulizi wa Arsenal na raia wa Gabon Pierre Emerick Aboumeyang amejiunga na Barcelona FC kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu huu.

⦁ Arsenal imenasa huduma za mlinzi Auston Trusty kutoka klabu ya Colorado Rapids.

⦁ Tottenham Hotspurs imepata sahihi ya Wachezaji Dejan Kulusevski, 21, kwa mkopo kutoka Juventus na Rodrigo Bantancur, 24, pia kutoka Juventus kwa mkataba wa kudumu.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *