Magazeti ya Jumatano Februari 2, 2022, yanaangazia ubabe wa kisiasa unaoshuhudiwa ndani ya muungano mpya wa Kenya Kwanza tangu Musalia Mudavadi ajiunge na naibu rais William Ruto.
Kuna taarifa pia kuhusu mabadiliko yanayotarajiwa kufanyika katika serikali ya Rais Uhuru Kenyatta huku waziri wake kadhaa wakitarajiwa kujiuzulu.
PEOPLE DAILY
Baadhi ya mawaziri kama vile Charles Keter wa ugatuzi, Peter Munya wa kilimo, Ukur Yatani wa fedha, Sicily Kariuki wa maji na wengine wanamezea mate viti vya kisiasa.
Rais Uhuru anatarajiwa kuwa katika hali ya kupanga serikali yake upya ili isiyumbe wakati mawaziri hao muhimu wataondoka.
Gazeti hili lina taarifa pia kuhusu mkurugenzi wa shule moja kaunti ya Mombasa ambaye amekamatwa kwa kumdhulumu mwanafunzi wa shule yake.
Inaarifiwa Nancy Gachewa wa shule ya Gremon aliwaongoza wanafunzi wengine kumpa kichapo Caleb Mwangi kwa madai ya wizi wa chapati.
Mwangi alidaiwa kuchukua chapati tano wakati wa chakula cha usiku badala ya moja kama walivyokuwa wameratibiwa.
The Standard
Taarifa kuu hapa ni kuhusu masaibu ambayo yameanza kudhihirika katika muungano mpya wa Kenya Kwanza.
Wakati wa kampeni Nairobii Jumanne Februari mosi, wagombea wa kiti cha ugavana Askofu Margret Wanjiru na Johnson Sakaja walizozana.
Mzozo ulishihudiwa katika bustani ya City ambapo vijana walimzomea Wanjiru alipokuwa akihutubu na kulazimu Sakaja kuchukua kipaza sauti.
Hata hivyo, hilo lilimkera Wanjiru ambaye alidai kuwa Sakaja anatumia genge la vijana kuwazomea mahasimu wake wa kisiasa.
Kwa dakika kadhaa, wawili hao karibu warushiane makonde katika kile kilionekana huenda kikamaliza uhusiano mwema miongoni mwa viongozi hao wa Kenya Kwanza.
Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.