Baada ya AFCON awamu ya robo fainali kukamilika na kuchukuwa mapumziko ya siku mbili, Leo grarambe hiyo inarejelea rasmi nusu fainali ambapo Burkina Faso itachuana dhidi ya Senegal.
Senegal wako katika nafasi nzuri ya kushinda AFCON mara yao ya kwanza katika historia yao, ila ni sharti wawapige Burkina Faso katika semi-fainali hii leo.
Senegal almaarufu The Lions of Teranga, waliingia nusu fainali baada ya kuwafunga Equatorial Guinea kwenye nane bora kwa ushindi mnono wa 3-1. Upande wao Burkina Faso, waliwafunga Tunisia 1-0 na kujikatia tiketi ya nusu fainali.
Mechi hiyo kati ya Burkina Faso dhidi ya Senegal, itaanza saa nne usiku saa za Afrika Mashariki.
Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.