Timu ya taifa ya Senegal almaarufu The Lions of Teranga imeingia fainali ya kombe la mataifa bingwa Afrika (AFCON) baada ya kuifunga Burkina Faso almaarufu Burkinabe 3-1.
Licha ya Burkinabe kujisatiti na kujituma vilivyo, Senegal ilizidi kubisha lango lao bila kuchoka.
Mabao kutoka kwa Abdou Diallo, Idrissa Gueye na mshambulizi wa Liverpool Sadio Mane yaliiwezesha Senegal kusonga mbele. Bao la peke la Burkina Faso lilifungwa na Bertranf Traore.
The Lions of Teranga itacheza fainali na mshindi kati ya Cameroon na Misri huku Burkina Faso itashindania nafasi ya tatu na timu itakayoshindwa katika fainali hiyo ya pili.
Senegal inaingia fainali mara ya pili mfululizo. Mwaka wa 2019 walishindwa na Algeria katika fainali.
Mechi hiyo kati ya Cameroon na Misri itachezwa saa nne usiku wa leo.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.