Ni rasmi sasa kwamba washambulizi Sadio Mane na Mohamed Salah, wote nyota wa timu inayocheza ligi kuu ya Uingereza, Liverpool, watakabana koo katika fainali ya AFCON.
Hapo jana Misri iliingia katika kilele cha mashindano hayo baada ya kuwacharaza wenyeji Cameroon 1-3 katika matuta ya penalti baada ya muda wa kawaida kuishia sare tasa.
Senegal walishinda Burkina Faso Jumatano baada ya kuwarindima 3-1 na kujibwaga katika fainali hii ya kukata na shoka ambayo itaandaliwa Jumapili saa nne usiku.
Mechi kusaka mshindi wa tatu na nne, ambayo itakuwa dhidi ya wenyeji Cameroon na Burkina Faso,itachezwa Jumamosi hii saa nne usiku.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.