Manchester United inazidi kupata wakati mgumu kulinda hadhi yake katika Premier League baada ya kutoka sare ya kufedhehesha dhidi ya Burnley jana jioni.
Licha ya Mashetani Wekundu hao kupata nafasi tele za kujikwamua sanasana katika kipindi cha kwanza, Burnely walionekana werevu zaidi kwao nyumbani na kuwashika mateka vijana hao wa Ralf Rangnick.
United walipata bao lao kupitia kiungo Paul Pogba dakika ya ’18 katika mechi iliyoshuhudia nyota Cristiano Ronaldo akikosa katika kikosi cha kaunza mchezo.
Kipindi cha pili, Burnley, wanaofunzwa na Sean Dyche, walikuja na mori na dakika ya 47 wakapata bao la kusawazisha kupitia Jay Rodriguez.
Wananyundo West Ham walipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Watford City kupitia Jerrod Bowen na kuvuka hadi nne bora.
Hii inaamanisha Tottenham Hotspurs, Man-Utd na Arsenal watazidi kuota kijibaridi nje ya nne bora.
Ligi hiyo inaendelea usiku wa leo ifuatavyo:
- Manchester City vs Brentford- 10:45pm
- Norwich vs Crystal Palace- 10:45pm
- Tottenham Hotspurs vs Southampton- 10:45pm
- Aston Villa vs Leeds United- 11:00pm
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.