EPL: Man-City yapanua mwanya kileleni kwa alama 12
Photo: Courtesy

EPL: Man-City yapanua mwanya kileleni kwa alama 12

Mabingwa watetezi Manchester City wamepanua mwanya kileleni mwa Premier League kwa alama 12.

City wamecheza mechi mbili zaidi ya Liverpool ambao wanashikilia nafasi ya pili na ambao leo watakuwa wanawakaribisha Leicester City katika mechi ya ligi kuu ya Uingereza.

Mabao kutoka kwa Riyad Mahrez na Kevin De Bruyne yaliwawezesha The Citizens kuponyoka na alama tatu muhimu.

Katika mechi zingine, Aston Villa walipiga sare ya 3-3 dhidi ya Leeds United. Matumaini ya Tottenham Hotspurs kumaliza nne bora yalizidi kutiwa doa baada ya kufungwa na Southampton 3-2.

Kwa sasa, Manchester City wanaongoza na alama 60, Liverpool 48, Chelsea 47 kisha West Ham United wanafunga nne bora na alama 40.

Club World Cup

Kule Abu Dhabi, mabingwa wa Ulaya, Chelsea, wamefuzu katika fainali baada ya kuifunga Al-Hilali 1-0. Bao la peke la Chelsea lilifungwa na raia wa Ubelgiji Romelu Lukaku katika kipindi cha kwanza.

Kwa sasa, vijana wake Thomas Tuchel watakabiliana na klabu ya Palmeiras kutoka taifa la Brazil, Jumamosi.

Picha: Romelu Lukaku [Hisani]

Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *