Masaibu yanayomkumba Zouma baada ya video akimdhulumu paka wake
Photo: Courtesy

Masaibu yanayomkumba Zouma baada ya video akimdhulumu paka wake

Kampuni maarufu kwa viatu vya wachezaji, Adidas, imesitisha mkataba wake wa kudhamini Kurt Zouma, beki mshambuliaji wa West Ham, baada ya video inayosambaa mtandaoni kuonysha akimdhulumu paka wake kwa kumkimbiza na kumpiga teke.

Taarifa ambazo sio rasmi zinaarifu kuwa kampuni ya Vitality pia imesitisha mkataba wao wa udhamini wa West Ham.

Klabu ya West Ham imemtoza faini ya pauni €250,000 Kurt Zouma na pesa hizo zitaenda kwa mashirika ya misaada ya Wanyama.

West Ham walichukua uamuzi wa kumpiga Zouma faini ya €250,000 jana na paka wake wawili wametunzwa na shirika la RSPEA ambalo ni shirika la ustawi wa Wanyama la Uingereza.

Katika taarifa rasmi, Adidas ilisema: “Tumehitimisha uchunguzi wetu na tunaweza kudhibitisha Kurt Zouma si mwanamichezo mwenye mkataba Adidas Tena.” 

Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji

Share this article
Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *