Magazetini: Waiguru aapa kumpa Uhuru funzo la kisiasa

Magazetini: Waiguru aapa kumpa Uhuru funzo la kisiasa

Magazeti yanaarifu kuwa Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru ameapa kumpa Rais Uhuru Kenyatta funzo la kisiasa ambalo hatathubutu kusahau.

Waiguru anadai eneo la Mlima Kenya lishasonga mbele sasa likiwa chini ya DP Ruto na kuacha mambo ya kizamani ya Uhuru

Waiguru alikuwa mwandani wa Uhuru lakini akaguria UDA ya Ruto mnano Oktoba 2021.

Ijumaa ya Februari 11, magazeti ya Kenya yaliripoti kuhusu siasa za urithi za mwaka 2022 ambapo Gavana wa Kirinyaga Anne Waiguru alidai kuwa chama tawala cha Jubilee ‘kilikufa na kikazikwa’.

Magazeti haya vilevile yanaarifu kuwa mwanafunzi anayekisiwa kuwa nyuma ya moto mkubwa ulioteketeza bweni la shule ya wasichana ya Moi, jijini Naiorbi, atahukumiwa mnano Februari 24.

Daily Nation

Gavana wa Kirinyaga Anne Waigiri ameapa kumpa Rais Uhuru Kenyatta funzo la kisiasa ambalo hatawahi kusahau katika uchaguzi mkuu wa 2022.

Waiguru, mwandani wa zamani wa kiongozi huyo wa taifa, aligura kambi ya Uhuru na kujiunga na UDA ya Ruto mnano Oktoba 2021 kwa kile kinachodaiwa kuwa shinikizo kutoka kwa wapiga kura.

Gavana huyo wa zamani wa Ugatuzi alisisitiza kuwa eneo la Mlima Kenya ambalo linajivunia ukwasi wa kura linaunga mkono azma ya urais ya Ruto na kuongeza kuwa kambi ya Azimio la Umoja inayoongozwa na kinara wa ODM Raila Odinga inarambishwa sakafu peupe katika uchaguzi mkuu wa Agosti 9.

Share this article
Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *