Magazeti ya Jumatatu, Februari 14, yanaripoti pakubwa kuhusu kampeni zinazoendelea za uchaguzi wa Agosti huku vyama pinzani vikipigana vita vya maneno.
Magazeti haya pia yanaripotia kuwa kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka anasemekana kutoa masharti fulani kabla ya kujiunga na Azimio la Umoja.
People Daily
Kulingana na gazeti hili, kiongozi wa Wiper, Kalonzo Musyoka amewasilisha mashati kadhaa kabla ya kujiunga na Azimio la Umoja, ambao Raila Odinga atatumia kuwania urais.
Magavana walioamua kujiunga na Azimio walisema Kalonzo amekuwa akiitisha huku viongozi wengine wakishabikia matakwa ya jamii zao.
Magavana Alfred Mutua (Machakos), Charity Ngilu (Kitui) na mwenzao wa Makueni, Kivutha Kibwana walisema wanaunga mkono Azimio ili kubadilisha maisha ya watu wa Ukambani.
Walimtuhumu Kalonzo kwa kujitenga na maslahi ya jamii ya Kamba ili kujifaidi yeye mwenyewe.
Imehaririwa na Ian Elroy Ogonji
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.