
Magazeti ya Jumatano Februari 16, 2022, yanaripoti kuwa rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wameamua kupakana tope katika siasa za urithi.
Kuna taarifa pia kuhusu kesi inayoendelea katika mahakama ya ICC ambapo wakili Paul Gicheru anakabiliwa na shtaka la kuwahonga mashahidi ili wajiondoe katika kesi zilizokuwa zikiwakabili Uhuru na Ruto.
Taifa Leo
Mwandishi wa gazeti hili anasema rais Uhuru na DP Ruto wamegeuka maadui kisiasa na sasa kila mmoja amesema atafichua siri chafu za mwenzake.
Viongozi wa chama cha Jubilee wanasema Kenyatta amepanga kuanza kampeni za kumchafua kisiasa Ruto katika ngome yake ya Mt Kenya. Katika safari hizo, wandani wa Kenyatta wanasema atafichua kilichosababisha talaka yao kisiasa.
Makamanda wa Ruto nao, wakiongozwa na mbunge Aden Duale, wanasema wao pia wako na ‘dirty files’ za Rais na akitoa za Ruto wao pia wanatoa zake.

Daily Nation
Taarifa yenye uzito hapa ni kumhusu DP Ruto baada ya kusema kuwa kinara wa ODM Raila Odinga ni miongoni mwa viongozi ambao walinufaika na sakata ya KEMSA ambapo mabilioni ya fedha yalitafunwa.
Ruto alimtaka rais Uhuru kuchapisha matokeo ya uchunguzi uliofanywa wakati wa sakata hiyo akisema yalikosa kuwekwa wazi kwa sababu marafiki wa Kenyatta wako ndani.


Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.