Wafanyibiashara wa kipato cha chini mjini Bungoma wanalalamikia ukosefu wa ufadhili wa mikopo ya kuendeleza biashara zao.
Wakiongozwa na Bi Violet Wakoli, wafanyibiashara hao wanasema imekuwa vigumu kwao kupata mikopo katika mashirika husika mjini humo. Wanadai mashirika hayo hayakubali wafanyibiashara wadogowadogo maana biashara zao ni ndogo mno na inabidi wao kuomba mikopo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Bi Wakoli anasema biashara zao zinakabiliwa na hatari ya kutoajiri watu wengine kwa kuwa hali ya uchumi ni mbaya.
“Changamoto zingine zinazoathiri wafanyibiashara wadogo ni miundo msingi duni, ukosefu wa rasilimali na ukosefu wa kuwepo kwa serikali kuwasaidia.
Biashara ndogondogo hazifai zidhalalishwe. Zinaweza kuwa uti wa mgongo na kurudisha hadhi ya uchumi wetu ambao umelemazwa na kurudi katika hali yake ya awali. Kwa hivyo, serikali iingilie kati na kufufua biashara hizi,” Bi Wakoli aliongezea.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.