
Magazeti ya Alhamisi Februari 24, 2022, yameupa uzito mkutano wa Sagana III ambapo Rais Uhuru Kenyatta alitangaza rasmi kuwa anamuunga mkono kiongozi wa ODM Raila Odinga kuwania urais.
Magazeti haya pia yamegusia kesi inayoendelea ya wakili Mkenya Paul Gicheru katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) ambapo alishtakiwa kwa kuwahonga mashahidi.
Daily Nation
Gazeti hili linaripoti kuwa Uhuru alizindua mashambulizi dhidi ya naibu wake William Ruto akieleza ni kwa nini alimpuuza kama mrithi wake na badala yake kumpendelea na kumuidhinisha Raila.
Akizungumza katika Ikulu ya Sagana State Lodge, rais alimuelezea naibu wake kama mtu asiyekuwa mwaminifu, akikosoa utendakazi wake chini ya usimamizi wake kama vile Kilimo kulingana na mpango wao wa kugawana madaraka mnamo 2013.

Vile vile alimushtumu Ruto kwa kuhujumu serikali yake kwa kususia kazi yake na kuanza kufanya kampeni zake za mapema ambazo Uhuru alisema hazijaathiri utawala wake.
Rais aliwaambia Wakenya kwamba Ruto anahusishwa na ufisadi na wizi wa pesa za mradi zilizokusudiwa kuwainua watu wa Mlima Kenya na kutoa pesa hizo kwa makanisa kama mchango.
Uhuru, bila kumtaja Ruto, alimhusisha na kashfa ya mabilioni ya mabwawa ya Kimwarer na Arror na kudai pesa zilizoibwa zilitumika kununua uungwaji mkono wa kisiasa katika Mlima Kenya, ikiwa ni pamoja na ule wa makasisi.
The Standard
Gazeti hili linaripoti kuwa Ruto ataanza ziara ya siku 12 nchini Marekani na Uingereza kuanzia Jumapili Februari 27, 2022.


Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.