Magazeti ya Jumatano Disemba 8 yanaendelea kuangazia siasa za uchaguzi mkuu ujao huku kinara wa ODM Raila Odinga akitarajiwa kuzindua rasmi azma yake ya kuwania urais Ijumaa.
Mkutano huo wa Raila unasubiriwa kwa hamu na ghamu huku wadadisi wakitarajia kuona iwapo vigogo wa muungano wa OKA Kalonzo Musyoka, Musalia Mudavadi, Moses Wetangula na Gideon Moi watahudhuria.
People Daily
Taarifa kuu kwenye gazeti hili ni kuhusu kualikwa kwa viongozi wa OKA kwenye kongamano la Azimio la Umoja katika uwanja wa Kasarani.
Raila ameandaa kongamano hilo ambapo anatarajiwa kutangaza rasmi kuwania urais 2022 na sasa maswali ni kuhusu msimamo wa vinara wa OKA.
Duru zinaarifu kumekuwa na presha kutoka kona kadhaa kwa vigogo hao wa OKA kumuunga mkono Raila.
People Daily inasema ni wajumbe 7,250 ambao wamealikwa Kasarani wakiwa ni kutoka kila wadi humu nchini.
The Star
Taarifa kuu kwenye gazeti hili ni kuhusu afisa wa polisi katili ambaye aliwapiga risasi watu watano kiholela Kabete.
Konstabo Benson Imbatu alichomoka kazini na bunduki aina ya AK 47 na kufika kwake ambapo alimpiga risasi na kumuua mkewe Carol Amagove.
Aliondoka nyumbani na kuenda akiwapiga risasi aliokutana nao katika kisa kilichowaacha watu watano wamefariki dunia.
Aidha, kuna taarifa kuwa mabwenyenye wa Mt Kenya Foundation wameamua kumuunga Raila Odinga mkono kuwania urais.
The Star iliripoti kuwa muungano huo umepanga kutoa uamuzi wake kabla ya Baba kutangaza kuwania urais Ijumaa Disemba 10
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.