
Mwanamume kutoka kijiji cha Butula katika eneo bunge la Budalangi, kaunti ya Busia, anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Port Victoria baada ya kujaribu kujitoa uhai.
Patrick Ouma, 32, inasemekana alimtuma mwanawe kununua wembe dukani na kuutumia kujipasua tumbo na kutoa matumbo yake nje kabla ya kupatikana na kukimbizwa ili kupokea matibabu ya dharura katika hospitali hiyo.
Naibu wa chifu wa kata hiyo John Odino amesema hadi sasa sababu ya Patrick kuchukua hatua hiyo bado haijajulikana.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.