
Ratiba ya timu zitakazo garagaza robo fainali ya Champions League [Picha-Hisani]
Droo ya robo fainali ya kombe la mataifa bingwa barani Ulaya almaarufu kama Champions League imeibua msisimko miongoni mwa mashabiki wa soka kote ulimwenguni.
Mpangilio wa ratiba ya mechi katika droo hiyo umechorwa ifuatavyo:
- Chelsea FC vs Real Madrid
- Manchester City vs Atletico Madrid
- Villarreal vs Bayern Munich
- Liverpool vs Benfica
Timu tatu (Liverpool, Chelsea na Manchester City) ni za Uingereza huku mbili (Real Madrid na Atletico Madrid) zikiwa za Uhispania. Benfica ni ya Ureno huku Bayern Munich ikiwa ya Ujerumani.
Mshindi wa robo fainali baina ya City na Atletico Madrid atakutana na mshindi wa robo fainali baina ya Chelsea vs Real Madrid katika nusu fainali ya kwanza.
Mshindi wa robo fainali baina ya Benfica na Liverpool atakutana na mshindi katika robo fainali ya Villarreal na Bayern Munich katika nusu fainali ya pili.
Mshindi wa nusu fainali ya pili atakuwa mwenyeji katika fainali.
Mechi za kwanza za robo fainali zitachezwa tarehe 5 na tarehe 6 Aprili na marudiano kufanyika tarehe 12 na 13 Aprili mwaka huu.
Mechi za nusu fainali ya kwanza ni tarehe 26 na 27 Aprili huku marudio yakiwa tarehe 3 na 4 Mei
Fainali itachezwa tarehe 28 Mei 2022 nchini Ufaranza.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.