Miamba wa Ulaya, Italia, wako nje ya Kombe la Dunia la mwaka huu nchini Qatar baada ya kupoteza 1-0 dhidi ya limbukeni Macedonia Kaskazini.
Macedonia Kaskazini waliwashangaza Italia na kusababisha miamba hao kukosa kombe la dunia kwa mara ya pili mtawalia tangu 1958 baada ya Aleksandra Trajkokski kutikisa wavu dakika ya 92.
Kwa sasa, limbukeni hao, baada ya ushindi huo, wamejikatia tiketi ya kufuzu kombe la dunia na watakutana na Ureno kwenye fainali kabla ya kuingia rasmi katika safari ya Qatar World Cup 2022 mwezi Novemba.
Italia walijaribu sana kwa kutuma makombora 31 langoni mwa wapinzani ila yote yalikuwa ni bure.
“Nimeshangaa sana. Sina la kusema. Wakati mwingine maajabu hufanyika kama vile yamefanyika usiku wa leo. Tulistahili kushinda ila wakati huu bahati haikuwa yetu. Pole sana kwa wachezaji wangu,” Mancini alisema.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.