Mwili wa mwanamume wa umri wa makamo asiyejulikana ulipatikana Jumamosi ukielea katika Mto Kipkaren.
Bi Florence Ayuma, mkaazi, alikuwa akirejea nyumbani Ijumaa jioni akiwa na wanawe kabla ya kuona kitu kikielea majini.
Mwili huo ulikuwa na majeraha mabaya. Inakisiwa kuwa huenda aliuawa na watu wasiojulikana kisha wakatupa mwili wake ndani ya maji.
“Tulidhani ni mti kwa umbali ila tukaona ni mwili wa mtu,” Bi Ayuma alihadithia West FM.
Naibu chifu wa Munyuki Bi Celestine Asige alithibitisha tukio hicho na kusema huenda mtu huyo aliuawa kwingineko na mwili wake ukasombwa na maji maana katika eneo lake hakuna kisa ambacho kimeripotiwa cha mtu kupotea.
Mwili wa mwendazake uliondolewa na maafisa wa polisi wa Lumakanda na unahifadhiwa katika hifadhi ya maiti ya Webuye.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.