Mataifa ya Ghana, Senegal, Cameroon, Morocco na Tunisia yatawakilisha Afrika katika Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Mechi kati ya Senegal na Misri ndio inayoangaziwa zaidi baada ya mshambulizi wa Liverpool Sadio Mane kufunga penalti ya mwisho na kuikatia tiketi The Lions of Teranka.
Mkondo wa kwanza uliishia 1-0 baada ya Muhammad Salah kuwapa Misri ushindi.
Mkondo wa pili, mechi hiyo muda wa kawada iliishia 1-1 ndipo ikaamuliwa kupitia mikwaju ya penalti.
Nyota wa Liverpool, Mohamed Salah, alipoteza penalti yake.
Timu zilizofuzu kutoka maeneo mengineo duniani ni ifuatavyo.
Ulaya
Ujerumani, Denmark, Ubelgiji, Crotia, Uhispania, Uingereza, Uswizi, Uholanzi, Poland, Ureno na Scotland/Wales.
Amerika Kusini
Brazil, Argentina, Ecuador, Uruguay, Peru, Colombia na Chile.
Asia na Australia
Korea Kusini, Iran, Japan, Saudi Arabia na Australia.
Amerika Kaskazini
Marekani, Mexico na Costa Rica zitapitia mchujo kabla ya timu moja kuwakilisha bara hilo.
Kombe la Dunia litaanza Novemba 21 nchini Qatar.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.