Vlabu vya Uingereza Liverpool na Manchester City vina kibarua kigumu usiku wa leo vitakapokuwa vikitafuta ubingwa wa Champions League katika robo-fainali mkondo wa kwanza.
Liverpool wanatarajia kuendeleza matokeo mazuri wakati wanawakaribisha vijana wa Benfica kutoka Ureno ugani Anfield mwendo wa saa nne, sawia na Manchester City watakaokuwa wakivaana na Atletico Madrid wa Uhispania.
Vijana wake Kloppe wamekuwa na matokeo mazuri siku za hivi karibuni na wikendi waliwanywika Watford City 2-0 katika kipute cha ligi kuu ya Uingereza na sasa wako alama moja tu nyuma ya vinara Manchester City jedwalini.
Liverpool wamekutana na Benfica mara nane. The reds wameshinda mara tano huku Benfica wakipata ushindi mara tatu. Liverpool wamefunga magoli 14 na Benfica wakifanikiwa kufunga mabao nane.
Mara yao ya mwisho kukutana ilikuwa msimu wa 2005/2006 raundi ya 16 bora ambapo vijana wa Benfica walipata ushindi wa 2-0 na kuwatupa nje Liverpool.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.