Leo saa kumi na mbili unusu ulimwengu mzima utasimama pale miamba wa soka Uingereza Liverpool watakuwa wanawakaribisha mabingwa watetezi Manchester City wa ligi kuu ya Uingereza katika kipute cha ubabe wa EPL.
Huku alama moja ikitenganisha timu hizi mbili katika jedwali licha ya kuwa Manchester City walikuwa wamepanua muanya alama 14 awali, leo ni siku ya kubaini nani mwenye sautinzito Uingereza msimu huu.
City wana alama 73 huku Liverpool wakiwafuata unyo unyo kwa alama 72.
Liverpool watakuwa wanatafuta ushindi wao wa tisa mfululizo huku City wakiwa wameshayumbayumba dhidi ya Tottenham na Crystal Palace katika mechi za awali.
Mechi hii moto itakuwa inaongeza uhasama kati ya Pep Guardiola na Jurgen Kloppe, mameneja wa City na Liverpool mtawalia.
Timu hizi mbili zimekutana mara 49 huku Liverpool ikiibuka na ushindi mara 20 na City wakishinda mara 11 na kupiga sare mara 18.
Mshindi wa leo atakuwa ameweka guu moja katika kunyakua ligi.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.