Kizaazaa kimeshuhudiwa katika kijiji cha Bwake, Trans Nzoia, baada ya wanywaji pombe ya kienyeji almaarufu changa’a kuvamia polisi ambao walikuwa katika harakati ya kukamata mgemaji.
Polisi hao inaarifiwa walifika bomani humo kwa nia ya kumtia mbaroni Bi Mulati ambaye alipiga mayowe ambayo yaliwavutia waraibu wa kileo chake na wenyeji ambao walikuja kwa wingi na kuzua vurugu.
Kwa mujibu wa ripoti ya polisi, ilibidi maafisa hao warushe vitoa majozi na risasi angani ili kutawanyisha umati ambao ulikuwa hatari kwa usalama wao.
Mvutano huo uliacha watu wawili wakiwa na majeraha mabaya na wanatibiwa katika hospitali ya rufaa ya Kitale.
Mwishowe, maafisa hao walifanikiwa kumnasa Bi. Mulati na mumewe na uchunguzi umeanzishwa ili kubaini chanzo cha mzozo huo.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.