Wikendi hii imeshuhudia matukio mengi viwanjani hasa katika ligi kuu ya Uingereza. Tumekusanya baadhi yake hapa.
Chelsea waporomoshwa kutoka kileleni na Wananyundo West Ham
Jumamosi jioni, Chelsea, almaarufu The Blues, walijutia kuzuru uga wa West Ham baada ya kuadhibiwa 3-2.
Vijana wa Tuchel walikuwa wa kwanza kuona lango la Wananyundo kupitia Mbrazili Thiago Silva kabla ya kiungo wa Italia Jorginho kupeana pasi mbaya iliyosababisha penalti. Kabla ya kipindi cha mapumziko, Mason Mount aliwaweka The Blues mbele.
Kipindi cha pili, vijana wake David Moyes walirudi kwa kishindo na wakapata bao la pili kupitia Bowen. Dakika za mwisho, Mausaka aliwapa West Ham bao la tatu na kuwahakikishia ushidi muhimu.
Kwa sasa Chelsea wamerudi hadi nafasi ya tatu na alama 33 huku Manchester City wakiongoza kwa alama 35, Liverpool wa pili na alama 34.
Origi aokoa The Reds dakika za mwisho
Liverpool, almaarufu The Reds, walikumbana na uzito wa Wanambweha Wolves Hampton ila dakika za mwisho Mbelgiji mwenye asili ya Kenya Divock Origi alifungia Liverpool dakika ya 93 na kuisaidia kupata alama 3 muhimu kwenye ligi kuu ya Uingereza ambayo imekuwa ngumu kwa sasa.
Manchester City kileleni
Jogoo wa mjini almaarufu The Citizens, Manchester City, wamevuka hadi kileleni mwa ligi baada ya kuwanyuka Wardford 3-1.
Vijana wake Pep walionekana kuwashinda maarifa vijana wake Cloudio Ranieri. Kwa sasa wanaongoza kwa alama 35.
Manchester United wapata ushindi wao wa kwanza chini ya mkufunzi mpya
Kocha Ralf RangRick ameanza maisha yake vyema kule jijini Manchester kwa kuibamiza Crystal Palace 1-0.
Crystal Palace ilikuwa imejikaza kutofungwa lakini mwishowe ikaitikia wito wa shetani mwekundu.
Kiungo Fred alifunga goli hilo la pekee la Red Devils na kuhakikisha wamepata ushindi wao wa pili mtawalia.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.