Man-Utd kuvaana na Arsenal katika vita vya nne bora
Kiashiria cha mtanange wa Man-Utd dhidi ya Arsenal [Picha-Hisani]

Man-Utd kuvaana na Arsenal katika vita vya nne bora

Man-Utd wana kibarua kigumu kujikwamua.

Vita vya nani atamaliza nne bora katika jedwali la Premier League vitapamba moto wakati ambapo Manchester United, yaani Red Devils, watakutana na Arsenal adhuhuri ya leo.

United, ambao wako chini ya kocha mpya Erik ten Hag, watakuwa wanajaribu kusahau madhila ya Jumanne usiku walipotingwa 4-0 na Liverpool watakapovaana na Arsenal leo saa nane unusu.

Vijana wake Mikel Arteta, Arsenal, yaani The Gunners, nao wana ari ya kuimarisha fahari yao hususan baada ya kuwafunga Chelsea 4-2 ugani Stamford bridge Juamatano usiku.

Arsenal wanashikilia nambari ya 5 na alama 57 huku Man-United wakiwa nambari ya 6 na alama 54. Kufikia sasa, The Gunners wamecheza mechi 32 na Red Devils 33.

Timu hizi mbili zimekutana mara 235, United wakiibuka na ushindi mara 100 huku Arsenal wakiponyoka na ushindi mara 85. Mechi ya mwisho Red Devils walitoka nyuma wakati ambapo nyota Cristiano Ronaldo alifunga mabao mawili na kuipa ushindi wa 3-2.

Iwapo United watashindwa mechi hii, basi uwezekano wao kukwea ngazi hadi nne bora utatiwa doa.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *