Ni majuma mawili tu Wakenya wameshuhudia uhaba mkubwa wa mafuta maeneo mbalimbali nchini, jambo ambalo lilipelekea serikali kuchukua hatua madhubuti kama vile kumfurusha mkuu wa kampuni ya Rubis kwa madai ya kulemaza uchumi maksudi kwa kuficha bidhaa hiyo muhimu.
Hata hivyo, aauzaji wa mafuta mjini Busia wamelalamikia kuendelea kwa hali hiyo kutokana na mgomo wa kampuni za petroli.
Wengi wa wahudumu wa pikipiki mjini humo wameonekana mchana wa leo wakiwa wamepanga foleni ndefu katika vituo vya Petro na Total, ambavyo ndivyo vilikuwa na mafuta pekee.
Michael Onyango, meneja wa kituo cha uuzaji mafuta cha Petro mjini Busia, amesema uhaba unaoshuhudiwa ni kutokana na kampuni ya Kenya Pipeline kufeli kusambaza mafuta ya kutosha kwa wanunuzi.
Meneja wa Kampuni ya Ola iliyo na tawi lake mjini Busia naye amedai kampuni za kusambaza mafuta ndizo za kulaumiwa.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.