Fifa yaadhibu Nigeria, Senegal na Algeria kwa utundu wa mashabiki
Salah akimulikwa miale ya katika mechi dhidi ya Senegal [Picha-Hisani]

Fifa yaadhibu Nigeria, Senegal na Algeria kwa utundu wa mashabiki

Fifa imetoa adhabu kali kwa timu tatu kwa utundu uwanjani.

Kumekuwepo na visa kadhaa vya kutatanisha kutoka kwa mashabiki wakati wa michuano ya kufuzu Kombe la Dunia raundi ya pili.

Kwa sababu hiyo, mataifa ya Nigeria, Algeria na Senegal wamepigwa faini na mafuruku kwa mashibiki wao na shirikisho la ulimwenguni FIFA baada ya mashabiki kutatanisha michuano hiyo Machi.

Katika uga wa Mashood Abiola, mashabiki wa Super Eagles ya Nigeria walikosa adabu timu yao ilipolemewa na Ghana na kutofuzu baada ya sare ya 1-1 na kushindwa katika matokeo ya jumla.

Kutokana na tukio hilo, Nigeria imepigwa faini na FIFA ya KShs 7,850,863 na watacheza mechi moja bila mashabiki.

Senegali nao wametozwa faini ya KShs 20,853,000 kwa kushindwa kuwazuia mashabiki wao ambao walionyesha boriti ya mwanga katika macho ya wachezaji kadhaa wa Misri akiwemo Mohamed Salah wakati wa mchuano wa raundi ya pili kule Dakar.

Mafarao wakishinda mchuano wa raundi ya kwanza Kwa bao moja na Lions of Teranga wakafaulu kushinda bao moja pia katika mchuano wa pili na ikalazimu wacheze dakika za nyongeza na hatimaye penalti.

Katika mikwaju ya penalti mashabiki wa Senegal walimulika miale ya miangaza katika macho ya Salah na akapoteza penalti yake.

Wenyeji waliishia kushinda katika mikiki ya hiyo ya penalti. Senegali pia watacheza mechi ijayo bila mashabiki.

Halikadhalika, Algeria imepigwa faini ya KShs 3,56,818 baada ya mashabiki wao kurusha vifaa na miale ya moto (fireworks) katika mchezo wao raundi ya pili dhidi ya Cameroon.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *