Sababu gani anjeti wa Toure alimlaani Pep Guardiola?
Pep Guardiola [Picha-Hisani]

Sababu gani anjeti wa Toure alimlaani Pep Guardiola?

Madai ya kulaaniwa kwa Pep yameibuka baada ya kupoteza mechi ya jana dhidi ya Real Madrid kiajabu.

Manchester City ilishuhudia maajabu usiku wa Jumatano ilipobanduliwa na Real Madrid kwenye nusu fainali ya Mabingwa Ulaya 2022 raundi ya pili ugani Santiago Bernabeu.

Real Madrid iliilowesha Manchester City mabao 3-1 na kufanya mambo 6-5 kwa jumla. Madrid ilichukua udhibiti wa mchezo kiajabu katika dakika mbili za mwisho za FIFA na wakafunga mabao mawili kwa haraka na kupelekea mechi hiyo kuingia muda wa ziada.

Mchezaji matata Benzema alitia kimyani penalti aliyozawadiwa baada ya kuchezewa visivyo katika lango la City.

Bahati mbaya ya Manchester City jana usiku imeibua minong’ono kuhusu swala la ubaguzi wa rangi lililopelekea mchezaji wa Kiafrika Yaya Toure kumlaani mkufunzi wa Man-City, Pep Guardiola.

Mnamo 2018, wakala wa Yaya Toure, Dmitri Seluk, alisema Guardiola hatawahi kushinda tena Ligi ya Mabingwa Ulaya kutokana na ‘uchawi’ wa Kiafrika wa “voodoo” ambao alisukumiwa baada ya kumdhulumu staa huyo wa Ivory Coast.

Yalianza yote wakati ambapo Pep Guardiola alimuuza Yaya Toure kwa klabu ya Manchester City 2010. Baadaye, Guardiola alijiunga na City 2016.

Pep alipotwaa usukani, Yaya Toure alianzisha tu mechi moja ya Ligi Kuu Uingereza na kucheza mechi kumi za ligi tofauti msimu wa 2017/2018. Jambo hilo lilipelekea Toure kumshutumu Guardiola kwa kutowapenda wachezaji wa Kiafrika.

Wapenzi wengi wa soka kote ulimwenguni wanaamini kuwa laana ya ajenti wa Toure imeanza kufanya kazi. Ajenti huyo alikuwa amelalamika kuwa Pep hakumpa Toure muda wa kutosha kucheza uwanjani.

Mashabiki wengi wa soka wamesema Guardiola anastahili kuomba msamaha kwa Toure baada ya Man-City kubanduliwa tena.

Ikumbukwe kuwa Pep amepoteza mara tatu tena kiutata katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya Toure na ajenti wake kutoa matamshi hayo.

Je, unaamini kwamba “voodoo” inapelekea bahati mbaya ya Pep?

Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *