Magazeti ya Ijumaa, Mei 13, yanaangazia taarifa kuhusu walio bora katika kuwa wagombea wenza wa Raila Odinga na William Ruto.
Aidha kuna taarifa pia kuhusu kikao cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika katika Ikulu Alhamisi Mei 12 ambapo uhusiano baridi uliendelea kushuhudiwa kati ya Rais na naibu wake.
Daily Nation
Gazeti hili linaripoti kuhusu utafiti wake wa ni nani anafaa kuwa mgombea mwenza katika miungano ya Kenya Kwanza na Azimio la Umoja.
Kwa mujibu wa utafiti huo, Martha Karua ndiye anapendelewa zaidi kama mgombea mwenza wa Raila Odinga ndani ya Azimio.
Kwa mujibu wa wafuasi wa muungano huo, asilimia 41 inasema Karua ni kiboko yao huku asilimia 27 ikimuunga mkono kinara wa Wyper Kalonzo Musyoka na kisha Peter Kenneth kwa asilimia 10.
Ndani ya Kenya Kwanza, Musalia Mudavadi ndiye chaguo huku akifuatiwa na Kindiki Kithure na kisha Gavana Ann Waiguru.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.