
Mchezaji nyota wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane [Picha-Hisani]
Mastaa wa Kiafrika wanatambulika kwa kutawala matukio muhimu katika soka ya ughaibuni. Wikendi iliyopita, wachezaji wa soka ya kulipwa wa Kiafrika walikumbana na bahati nzuri na mbaya kama inavyoelezwa na Robert Mutasi.
Sadio Mane apoteza penalti
Licha ya kushinda kombe la FA dhidi ya Chelsea, ilikuwa kubaya kwa raia wa Senega, Sadio Mane, ambaye alipoteza mkwaju wa penalti katika matuta baada ya muda wa kawaida na ziada kufel kutoa mshindi.
Edourdy Mendy aliokoa penalti yake Mane ambayo ilikuwa ya tano na yenye kuamua ushindi wa Liverpool.
Licha ya Mane kupoteza, miamba hao wa soka kutoka Merseyside waliishia kushinda mikiki hiyo ya penalti 6-5.
Jeraha la Salah
Mohamed Salah alijeruhiwa dakika ya 33 katika mechi hiyo na kuondolewa uwanjani, jambo ambalo liliathiri mfumo wa nahodha Jurgen Klopp. James Milner alichukua nafasi yake Keita na Matip akachukua mahala pa Virgil van Dijk baada ya Jurgen Klopp kufanya mabadiliko dakika ya 90 huku Mmali Ibrahima Konate akicheza mwanzo hadi mwisho.
Mabao ya Taiwu Awoniyi
Staa wa Nigeria Taiwu Awoniyi alifunga mabao mawili baada ya Union Berlin kushinda 3-2 dhidi ya Bochum katika mechi yao ya mwisho Bundesliga.
Awoniyi aliongezea Berlin bao la pili kutoka maeneo ya penalti dakika ya 25 kabla ya kufunga bao la tatu dakika ya 88 na kumaliza msimu katika nafasi ya tano kwa alama 57.
Madhila ya Edourd Mendy na Hakim Ziyech
Mendy na Ziyech walionyesha mchezo mzuri katika mchuani wa FA isipokuwa Chelsea mwishowe walishindwa.
Mendy alipangua mikiki kabla ya matuta ya penalti na baadaye na baadaye kuukaba wa Mane.
Licha ya Ziyech kufunga mojawepi ya penalti ya Chelsea, juhudi ziliambulia patupu baada ya Liverpool kubeba kombe Wembley.
Weledi wa Jeffrey Schlupp
Wawili hawa waliunganisha nguvu zao pamoja na kuwezesha Crystal Palace kusawazisha katika dakika ya 81 dhidi ya Aston Villa.
Villa ilikuwa imeongoza dakika ya 68, lakini Schlupp alipokea pasi kutoka kwa Guehi dakika za mwisho kipindi cha pili. Schlupp alisawazisha dakika 3 na sekunde 37 baada ya kuingia kama nguvu mpya.
Kwa sasa amefunga bao la tano katika ligi akitokea kwenye benchi ya mabadiliko kwa Palace.
Bahati mbaya ya Riyadh Mahrez
Mualjeria Riyadh Mahrez alipoteza penalti ya Manchester City katika mechi iliyoishia sare ya 2-2 dhidi ya West Ham United.
Mahrez sasa amepoteza penalti mbili katika michuano yote ya Manchester City. Ya kwanza ilikuwa dhidi ya Liverpool mnamo 2018, lakni amefunga penalti 9.

Thanks for choosing WKT. Advertise with us for affordable offers.