Mutuma: Vijana waandaa soka ya kuhamasisha amani musimu huu wa siasa
Wachezaji wa Undugu na 11 Stars katika mechi ya awali [Picha-Tom Lutali, WKT]

Mutuma: Vijana waandaa soka ya kuhamasisha amani musimu huu wa siasa

Timu sita zinashiriki shindano hilo.

Kama njia mojawapo ya kudumisha amani msimu huu wa siasa, timu sita katika kijiji cha Mbagara, wadi ya Mautuma, Lugari, zimekuja pamoja ili kuwaleta vijana pamoja msimu huu wa siasa.

Timu hizo ni Undugu FC, Bafana FC, Ivona East, Mukonge, Tebuka na 11 Stars zimechangisha kila timu KShs 600 ili kuwaleta vijana pamoja msimu huu wa siasa na wakati ambapo wanafunzi wako katika likizo fupi.

“Vijana wengi hutumiwa na wanasiasa kuzua vurugu katika mikutano ila maswala hayo tunataka kuyaweka katika kaburi la sahau kwa kuandaa soko hii hapa Mbagara Primary,” muasisi wa kipute hicho, mwalimu Barnabas Barasa, alisema.

Aliongezea kuwa hii ni fursa nzuri sana ikizingatiwa Mautuma ni eneo ambalo lina makabila yote kwa hivyo itakuwa vyema kukihubiriwa amani sasa kupitia mchezo wa soka.

Waandalizi hao wanatoa wito pia kwa viongozi wa eneo hilo iwapo wana nia ya kuhubiri amani wajiunge nao ili kuleta jamii zote eneo hilo pamoja.

Mshindi wa shindano hilo la Mautuma Soka Bonanza atatia kibindoni KShs 5,000.

Kilele cha mechi hizo Jumapili hii ijayo katika uwanja wa shule ya msingi ya Mbagara Primary.

Ratiba ya mechi za leo:

  • Mkonge vs Tebuka
  • 11 Stars vs Ivona East
Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *