Maafisa wa polisi eneo la Panpaper mjini Webuye wamemkamata mzee wa miaka 55 akisafirisha kilo 550 ya misokoto ya bangi yenye thamani ya mamilioni ya pesa katika magunia.
Akidhibitisha kisa hicho, kamanda wa polisi eneo hilo la Webuye Kaskazini, Gloria Ng’etich, amesema ushirikiano kati ya maafisa wake na wale kutoka kaunti ya Kakamega uliwawezesha kumnasa mshukiwa.
Mzee huyo alikamatwa mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi katika barabara kuu ya Malaba-Eldoret baada ya wananchi kuarifu polisi.
Mshukiwa atasalia kizuizini akisubiri maafisa wa polisi wamalize uchunguzi kisha afikishwe mahakamani.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.