Sports Roundup: Penalti zilizookoa Chelsea, Liverpool, City na United
Wachezaji wa Manchester City wakisherehekea baada ya kufunga goli. (Picha- hisani)

Sports Roundup: Penalti zilizookoa Chelsea, Liverpool, City na United

Wikendi hii imeshuhudia mambo ya kusisimua viwanjani hasa katika ligi kuu ya Uingereza. Timu kuu zote za Uingereza zilipata penalti ambazo zimesaidia vilabu hivyo kutoka midomoni mwa wapinzani wao.

Manchester City yailabua Wolves Hampton 1-0

Bingwa mtetezi Manchester City alikumbana na upinzani mkali kutoka kwa mbwa mwitu Wolves Hampton ugani Etihad Stadium.

City, almaarufu The Citizens, walionekana kumiliki mpira kwa asilimia kubwa ila kupenya ngome ya Wolves ilikuwa ngumu. Kipindi cha kwanza, timu hizo ziliachana 0-0. Kipindi cha pili, City walipata penalti baada ya wing’a Raheem Sterling kuchezewa vibaya kisha yeye mwenyewe akachukua penalti hiyo na kufunga. Bao hilo lilikuwa lake la 100 akiwajibikia Manchester City.

Raheem sterling akisheherekea bao lake. (Picha- Hisani)

Baada ya ushindi huo, City wangali kileleni mwa ligi na alama 38, alama moja tu mbele ya Liverpool.

Salah awaondolea Liverpool aibu

Mjukuu wa Pharaoh Mohammed Salah aliokoa vijana wake Kloppe baada ya kupata penalti na kuwafungia dhidi ya Aston Villa.

Picha Muhammad Salah akisheherekea bao lake. (Picha- Hisani)

Licha ya Aston Villa kuonyesha nia, bidii yao iliambilia kipigo cha 1-0.

Chelsea waponea dakika za mwisho

Chelsea, walijikuta wako chini bao moja sufuri baada ya Marcos Alonso kumchezea Raphina visivyo kisha akazawadiwa penalti ambayo yeye mwenyewe alifunga.

The Blues waliendelea kubisha dakika ya 36′, Marcos Alonso, alimpa pasi Mason Mount kisha akasawazisha. Kipindi cha pili, Antonio Rudger alichezewa vibaya na Raphina kisha Jorginho akafunga la pili. Mshambulizi wa Leeds United alifungia wageni bao la pili na mambo yakawa 2-2. Dakika ya 91, Rudger alichezewa vibaya tena Jorginho akaja mara ya pili na kufunga penalti na mambo yakawa 3-2.

Antonio Rudiger akisherehekea baada ya kufunga penalti. (Picha- Hisani)

Arsenal waiburura Southampton 3-0

Arsenali waliendeleza matokeo mazuri baada ya kuadhibu Southampton 3-0. Alexander Lacazette, Gabriel Matineli na Orghaard walifungia washika bunduki bao moja kila mmoja na kuweka hai matumaini ya vijana hao wa Michael Arteta kuingia nne bora.

Penalti ya Ronaldo yainusuru United

Baada ya kutoka sare katikati mwa juma dhidi ya Young Boys katika UCL, vijana wake Ralf Rangnick waliendeleza ushindi wao wa pili wa ligi chini ya mkufunzi huyo dhidi ya limbukeni Norwich City.

Mreno Cristiano Ronaldo alichezewa vibaya dakika ya 76 kisha akafunga penalti aliyozawadiwa mwenyewe.

Mechi zingine: Kwingineko Leicester City iliifunga Newcastle United 4-0 huku Westham United ikitoka sare na Brighton 0-0. Crystal Palace nao walizidisha machungu ya Everton baada ya kuwafunga 3-1.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *