Disemba ni mwezi wa mwisho wa mwaka ambao unajulikana hususan kwa sherehe za Kikristo za Krismasi ambazo kilele chake ni tarehe 25 kuadhimisha kuzaliwa kwake Yesu Kristo.
Lakini je, wafahamu kuwa kuna sherehe zingine nyingi maalum ambazo huadhimishwa mwezi huu huu kote duniani? Tom Lutali ametuandalia makala kuhusu baadhi ya sherehe hizi.
Sherehe za De Santo Tomas, Guatemala
Sherehe hii huadhimishwa kuanzia tarehe 13 mpaka 21 na hufanyiwa juu ya mlima upande wa kaskazini mwa nchi ya Guatamala, kando ya ziwa Atitlan. Jiji la bara la Chichicatenango na pahali pa sherehe za kanisa hufana kwa watu kucheza na kuruka.
Siku kuu hii hufika kilele tarehe 21 baada ya wiki mzima ya kucheza gwaride na miale ya moto, huku mti mrefu ukiwekwa ukiwa umefungwa kwa kamba; wenyewe wakiukwea kwa madaha kuashiria kuwa majaribio yameisha.
Sherehe za Hanukkah, Israeli
Zinaitwa pia sherehe za Mwangaza. Sherehe za Hanukkah huadhimishwa kuanzia tarehe 10 mpaka 18 kwa madhumuni ya kuosha dhambi.
Maadhimisho haya, ambayo hufanywa hekaluni, ni ukumbusho wa vita vya Wayahudi dhidi ya Wagiriki mwaka wa 165 BC.
Mshumaa mmoja huashwa kila siku wakati wa Hanukkah. Hii inaafikiana na wakati wa vita ambapo Wayahudi walichoma mishumaa kwa siku nane na mafuta kwa siku moja. Katika sikukuu ya Hanukkah, vilevile, nyimbo huchezwa na Wayahudi kubadilishana zawadi kuonyesha umoja wao.
Los Posades, Latin
Los Posades ni jina la Kilatino, maana yake kuongeza maombi. Sherehe hii huadhimishwa sana katika mataifa yaliyo na watu wa asili ya Kilatino: Mexico, Guatamala, Cuba, Uhispania na Amerika.
Sikukuu hii inayosherehekewa kati ya tarehe 16 na 24 huwa ukumbusho wa Maria mama yake Yesu Kristo. Watu huimba na kula pamoja kuonyesha upendo.
Kwanzaa, Marekani
Sherehe za Kwanzaa zilihasasiwa na Dr Maulana Karenga mwaka wa 1966 baada ya mapigano ya Watts Riot mjini Los Angeles, Marekani. Sherehe zilianza na mila za Kiamerika kisha za Kiafrika.
Jina la sherehe hizi lina maana ya ‘matunda ya kwanza’.
Sikukuu hii huhusisha nyimbo, kucheza na vyakula vya kitamaduni. Katika siku saba, familia hujikusanya pamoja na kuwasha mishumaa; maana yake ni watu kujitegemea, kuwajibika na kuishi kwa amani.
Sherehe ya Siku Tatu za Mfalme, Uhispania
Baada ya siku kumi na mbili za Krismasi, inakuja siku inayoitwa Epiphany au Siku Tatu za Mfalme inayoadhimishwa Uhispania.
Siku hii inasherehekewa baada ya watu ‘kuona Kristo’ na ‘kumpa zawadi’. Watoto wengi hupewa zawadi jijini Peurto Rico. Kabla ya mtoto kuenda kulala mnamo Januari 5, watu huacha kateni ya nyasi kitandani pake, kuashiria kuwa Mfalme atapata zawadi nono.
Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.