Magazetini: Vita Bungeni kuhusu hoja ya Azimio

Magazetini: Vita Bungeni kuhusu hoja ya Azimio

Magazeti ya Jumanne, Disemba 21, yanaripoti kuwa wabunge wanakabiliana katika vita vya ubabe wa kisiasa huku Bunge likijadili mswada tatanishi kuhusu vyama vya kisiasa ambao utaruhusu Azimio La Umoja kualika vyama vidogo kuelekea uchaguzi wa urais.

Magazeti haya pia yanaripoti kwamba Marekani imesitisha kwa muda huduma za utoaji visa hadi Januari 23, huku Dubai ikipiga marufuku ndege kutoka Kenya sikukuu ya Krismasi inapokaribia.

The Standard

Mpango wa rais Uhuru Kenyatta na kinara wa Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga kufanyia sheria marekebisho na kubuni mrengo wa kisiasa kama Narc ili kuchukuwa hatamu za uongozi 2022 umeibua vita vipya kisiasa ambavyo vitajitokeza katika kikao cha leo Bungeni.

Washirika wa naibu rais William Ruto jana waliapa kutia kila jitihada kuzuia mabadiliko yoyote yaliyopendekezwa kubuni mrengo wa kisiasa wa Coalition Political Party (CPP).

Mpango huo wa kaka wawili wa handisheki unalenga vyama vya kisiasa kumteua mgombea wao pamoja kote nchini chini ya mrengo huo ambao bado haujasajiliwa.

Lengo kuu ni kuzuia vyama kumezwa na wawaniaji wanaounga mkono vuguvugu la Azimio La Umoja, ambalo Raila anatumia kama ala ya kampeni zake za urais.

People Daily

Siku ya Jumatatu, Marekani ilisitisha kwa muda huduma ya utoaji wa visa duniani huku serikali ya Dubai ikipiga marufuku ndege za kutoka Kenya kwa saa 48, kirusi cha Omicron kikiendelea kuhangaisha usafiri kote duniani.

Masharti ya Marekani na Mamlaka ya Uchukuzi wa Ndege Dubai (DCAA) yanawadia siku moja baada ya makali ya COVID-19 kuongezeka hadi 29.6%, kutoka 24.4% iliyosajiliwa Jumapili.

Serikali ya Marekani ilisema itasitisha huduma za visa kuanzia Disemba 20, 2021, hadi Januari 3, 2022, hatua ambayo itawaathiri Wakenya wanaotaka kusafiri nchini humo kwa sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *