Kimeumana: Ndivisi Younsters kupima tajriba ya Ndivisi United Jumapili
Kikosi cha Ndivisi United | Hisani

Kimeumana: Ndivisi Younsters kupima tajriba ya Ndivisi United Jumapili

Jumapili Disemba 26, 2021 ni siku ambayo mashabiki wa kandanda eneo la Ndivisi na viunga vyake watakuwa wanashuhudia debi ya kukata na shoka kati ya Ndivisi United almaarufu ‘Wazee wa Kazi’ na vijana chipukizi Ndivisi Youngsters almaarufu ‘Juniors’.

Debi hii ya Webuye Mashariki katika kaunti ya Bungoma inatazamiwa kuwa ngumu kwa pande zote mbili ikizingatiwa kila upande una ari ya kuonyesha ubabe wake mwaka wa 2021 unapokamilika.

Ad

Mchwano huu wa kufana umedhaminiwa na baadhi ya washikadau wa kandanda eneo hilo. Mshindi anatarajiwa kupata kitita cha KSh 30,000 huku wa pili akipokea KSh 20,000.

Uwezo wa Ndivisi Youngsters

Mechi hii itakuwa na msisimuko wa aina yake, ikizingatiwa Ndivisi Youngsters wana kikosi ambacho kina uzoefu wa mchezo. Wanajivunia wachezaji wa haiba yake kama vile mlinda lango hatari Jimmy ambaye ni mzuri kwa kuokoa penalti.

Pia kuna Samuel Lusweti ambaye ni mweledi wa kufunga kutumia kichwa.

Kikosi cha Ndivi United kikifurahia hali | Hisani

Safu ya kati inaongonzwa na Francis Chesimei, fundi wa kupiga pasi nyerezi na chenga za kimaudhi akisaidiwa na Ben Simiyu. Safu ya ushambulizi inaongozwa na Peter Kakai.

Umri mdogo katika timu hii ya Ndivisi Youngsters unawapa ari zaidi ya mchezo huu kwa kuwa wana uwezo wa kustahimili presha ilinganishwa na wale wa United.

Ubabe wa ‘Wazee’

Kikosi cha Ndivisi United kinashirikisha wachezaji waliovuma siku za hapo awali. Wengi wao waliweza kustaafu ila wengine wamekuwa wakicheza na vijana wa Juniors na kumekuwa na upinzani mkali kati yao.

Ndivisi United wanajivunia wachezaji ambao wemecheza katika viwango vya juu na wana tajriba ya hali ya juu ikilinganisha na wale wa Ndivisi Youngsters. Baadhi ya wachezaji ni beki mchapa kazi Ingana Khakame na James Situma ambaye ni mojawapo ya vijana wa nyumbani ambao wamecheza hadi ligi kuu nchini.

Ad

Kuna pia Simeon ambaye ni kiungo hatari anayesifiwa kwa kudhibiti kiungo cha kati anapocheza, bila kumsahau David Rasto ambaye anasifika kwa kuwachilia fataki za mbali akilenga lango.

Kocha wa Ndivisi United ana matumaini makubwa kwa kikosi chake anachoamini hakitingiziki.

“Najiamini na kikosi hiki, ni wakongwe ila wanasema simba mwenda pole ndiye mula nyama, kikosi cha Juniors tunakifahamu na tunajua jinsi wanavyocheza, wako na kasi lakini sisi tutatumia uzoefu na tajriba tuliyo nayo na nina uhakika tutashinda,” alisema.

Kwa kweli debi hio itafanya heshima iwepo, je itakuwa baba kumpa heshima kijana?

Ad


Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *