Matukio katika Premier League wikendi hii

Wikendi hii ya mwisho wa mwaka wa 2021 imekuwa na matukio kadhaa ya kusisimua katika ligi kuu ya Uingereza.

Picha | Getty Images

Manchester City yailabua Leicester City 6-3

Vinara wa ligi kuu ya Uingereza Manchester City wanazidi kuendeleza matokeo mazuri baada ya kuwafunga Leicester City 6-3 ugani Etihad Stadium. Kwa sasa, City wanaongoza kwa alama 47, alama sita mbele ya Liverpool ambao wanashikilia nafasi ya pili huku mechi yao ikiahirishwa kutokana na virusi vya Corona. Liverpool wana alama sawia na Chelsea, ila The Blues wanadunishwa na mabao.

Arsenal yaifungwa Norwich City 5-0

Licha ya kuanza msimu na kusuasua, vijana wake Arteta wameonyesha nia ya kumaliza nne bora. Mabao mawili kutoka kwa kinda wa timu ya taifa ya Uingereza Saka, moja kutoka kwa Lacazette, lingine kutoka kwa Rowe na Gabriel Matineli, yaliiwezesha Wanabunduki kuponyoka na alama tatu muhimu. Kwa sasa wako nafasi ya nne na alama 35.

( Picha Saka akisheherekea bao lake)

Chelsea wajiondolea aibu

Mechi tatu zilizopita, vijana wake Thomas Tuchel wamekuwa wakisuasua ila leo wamejikwamua ugenini baada ya kuwafunga Aston villa 3-1.

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Italia Jorginho alifunga mikwaju ya penalti miwili, moja baada ya Odoi kuangushwa, kisha nyingine kutoka kwa mshambuliaji Romelu Lukaku. Lukaku alifungia Chelsea bao la pili na kuzalisha lingine. Bao la Aston Villa lilifungwa na Reece James.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *