Morocco yabeba dua ya Afrika katika makabiliano na Ufaranza
Morocco kutoana kivumbi leo na Ufaranza/Hisani

Morocco yabeba dua ya Afrika katika makabiliano na Ufaranza

Morocco ndio timu ya kwanza ya Afrika na Uarabuni kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Leo usiku saa nne kamili, vijana wa timu ya taifa ya Morocco, almaarufu The Altas Lions, watashuka ugani Al Bayt nchini Qatar kupeperusha bendera ya Afrika watakapo vaana na Ufaranza, yaani Les Bleus (Wanasamawi), katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Dunia.

Morocco wamefungwa bao moja tu katika mechi sita na ilikuwa dhidi ya Canada ambapo walipata ushindi wa 2-1.

Mkufunzi wa Morocco, Walid Regragui, alisema Jumanne kwamba kufika kwa timu yake nusu-fainali si chochote na wanatumai kuwapa Wafaranza wakati mgumu.

Ufaranza wanaonekana kupigiwa upato kunyakua kombe hilo kwa mara ya pili mfululizo. Walituzwa mabingwa wa Kombe la Dunia mwaka wa 2018 walipowashinda Croatia katika fainali nchini Urusi.

Morocco walitinga nusu-fainali baada ya kuwafunga Uhispania 4-0 kupitia matuta ya penalti.

Kwa upande wao, Ufaranza waliwaadhibu Uingereza 2-1 na kujikatia tiketi ya nusu-fainali.

The Atlas Lions ndio timu ya kwanza ya Afrika na Uarabuni kutinga nusu fainali ya Kombe la Dunia lenye miaka 92.

Morocco imeangusha miamba wa Ulaya: Ubelgiji, Uhispania na Ureno katika safari yake angavu ya Qatar 2022.

Share this article

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *