
Kenyan newspapers today/Courtesy
Magazeti ya Alhamisi, Januari 5, yanaripoti kwa upana kuhusu mahojiano ya Rais William Ruto na wanahabari kutoka vituo mbalimbali humu nchini.
- The Star
Chapisho hili linaripoti kuwa mama mmoja kutoka eneo la Ndiwa alikamatwa kwa madai ya kuchoma mikono ya mwanawe kwa kuiba Sh50.
Polisi wa Ndhiwa walimkamata na kumhoji mwanamke huyo kwa kuchoma mikono ya mtoto wake wa miaka tisa.
Mwanamke huyo alimshutumu mwanawe, ambaye ni mwanafunzi wa Gredi ya 4, kwa kuiba pesa na kununua chakula katika soko lililo karibu.
Majirani wanaoifahamu familia hiyo walisema mvulana huyo amekuwa akikabiliwa na njaa tangu mwanamke huyo alipoolewa na mwanamume mwingine baada ya babake mvulana huyo kufariki.
Alipokamatwa Jumanne, mwanamke huyo aliwaambia maafisa wa polisi kwamba mvulana huyo alikuwa akiwaibia hata majirani zao licha ya kumuonya mara kadhaa.
Kukamatwa kwake kulijiri baada ya polisi kupata habari kuwa mwanamke huyo alimfungia mwanawe ndani ya nyumba baada ya kuchoma mikono yake.
Chifu wa eneo la Lower Kayambo, Cyprian Obonyo, alisema walimkamata mwanamke huyo na kumpeleka katika kituo cha polisi cha Ndhiwa.
- Daily Nation
Katika gazeti hili, polisi, afisa wa Bunge la Kaunti ya Nyamira, afisa wa Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) na muuguzi ni miongoni mwa washukiwa wakuu wanaochunguzwa kuhusu mauaji ya kinyama ya mwalimu wa Nyamira.
Mwili uliokatwakatwa wa mwalimu mkuu wa Shule ya Msingi ya Getengereirie, Ezekiel Nkeere Gitangwa, ulipatikana katika nyumba ya muuguzi huyo siku ya Jumapili.
Maafisa wa polisi bado wanamsaka muuguzi huyo ambaye wanamchukulia kama mshukiwa mkuu. Siku ya Jumatatu, walimtaka ajisalimishe kwa kituo cha polisi kilicho karibu.
Kulingana na gazeti hili, wanaume hao watatu, ambao sasa wako katika rada ya polisi, walikuwa wageni wa muuguzi huyo kila mara.
Kwa upande wa afisa wa NYS anayesemekana kuwa mpenzi wake muuguzi huyo, majirani wanasema alionekana katika nyumba hiyo siku moja kabla ya kisa hicho.
Inasemekana kuwa afisa huyo wa NYS alimtembelea muuguzi huyo mnamo Alhamisi, Disemba 29, na kushinda huko siku nzima.
Mnamo Ijumaa, Disemba 30, 2022, mwalimu huyo alitoweka na majirani walisikia zogo kutoka kwa nyumba hiyo, kakake marehemu James Maganda alidai.
- The Standard
Chapisho hili linaripoti kuwa kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka ameunga mkono pendekezo la Rais William Ruto la kubuniwa rasmi kwa wadhifa wa kiongozi wa upinzani.
Mnamo Disemba mwaka jana, Ruto aliwasilisha risala mswada Bungeni akiwataka wabunge kurekebisha Sura ya 9 ya Katiba ili kubuni rasmi Afisi ya Kiongozi wa Upinzani.
Alisema kuwa kuanzishwa tena kwa nafasi ya kiongozi huyo hakuwezi kudhibiti utawala wake bali kutaweka utawala wake kuwa makini kutekeleza wajibu wake kidemokrasia.
Kiongozi wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga, hata hivyo, alionya kuwa hatakuwa mwepesi kuunga mkono sheria inayopendekezwa, akibainisha kuwa mrengo wake utachunguza kwanza yaliyomo kwenye mswada huo na kuukataa iwapo ni kinyume cha Katiba.
Lakini katika mahojiano, kiongozi wa Wiper aliunga mkono hatua hiyo akisema itaimarisha demokrasia.
Vile vile alipuzilia mbali madai kuwa aliviziwa na Ruto ili ajiunge na utawala wake wa Kenya Kwanza katika wadhifa wowote.
4. Taifa Leo
Gazeti hili linaripoti kuhusu wahudumu wawili wa bodaboda ambao wameshtakiwa kwa ujambazi. Wawili hao, ambao wanadaiwa kuwa katika genge la majambazi lililojumuisha afisa wa polisi aliyeuawa kwa kupigwa mawe mkesha wa sikukuu ya Krismasi, wameshtakiwa kwa wizi wa kimabavu.
Genge hilo lilikuwa likiwavamia wakazi wa Kilimani na kuwaibia mali zao mnamo Disemba 24, 2022, wakati walifumaniwa na wananchi na kumuua Konstebo Ken Kavulanga kwa mawe na vifaa butu.
Hata hivyo, John Kyalo Makau, almaarufu Jonte, na Thomas Malusi Kilonzo, almaarufu Bosco, walifaulu kutoroka kwa pikipiki.

Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.