Magazeti ya Alhamisi, Januari 12, yameangazia mfumo mpya wa ushuru, na pia mageuzi yaliyopendekezwa na Rais William Ruto katika Huduma ya Kitaifa ya Polisi (NPS).
Taifa Leo
Gazeti hili linaripoti kuwa wachungaji watatu walifikishwa katika mahakama ya Eldoret, Jumatano, Januari 11, kwa kumiliki bunduki mbili ya AK47 na risasi nane.
Titus Kipruto, Caleb Nyongesa na Frankline Kipruto waliokamatwa Disemba 2022, walishtakiwa kwa kumiliki bunduki bila leseni.
Watatu hao wanaripotiwa kwamba walipatikana Disemba 2022, na bunduki aina ya AK47 katika kaunti ndogo ya Kapseret bila leseni.
The Star
Kulingana na gazeti la The Star, aina mpya ya ugonjwa wa kisonono umekita kambi jijini Nairobi na kuhatarisha maisha ya wengi.
Wataalamu wameelezea wasiwasi wao huku wakifichua kuwa wakazi wengi wa mijini wanaugua ugonjwa huo ambao unahatarisha sana afya yao ya uzazi.
Matokeo hayo yametokana na utafiti uliofanywa mwaka jana baada ya sampuli kuchukuliwa kutoka kwa kahaba mwenye umri wa miaka 24.
Watafiti walisema kwamba wanaougua ugonjwa huo ni nadra sana konyesha dalili zozote.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.