
Mkufunzi wa Man United Eric Ten Hag/Hisani
Wachezaji wa Manchester United wamefika katika uwanja wa mazoezi saa moja asubuhi baada ya kipigo cha aina yake cha mabao saba bila jibu katika mechi dhidi ya Liverpool ugani Anfield Jumapili.
Kocha Eric Ten Hag anasemakana kufika saa mbili mapema kabla ya wachezaji wa Red Devils.
Ten Hag aliwahimiza vijana wake kurudisha imani ya mchezo licha ya kuhujumiwa na wapinzani wao wa jadi.
United walikuwa tu ndio bado wanasherehekea ushindi katika kombe la Carabao dhidi ya Newcastle. Walikuwa wameshindwa tu mechi moja kati ya 22 kabla ya kichapo cha Liverpool.
Tangu mwezi Disemba mwaka wa 2007, Manchester United imeshinda mechi tatu pekee ugani Anfield, na mara ya mwisho walishinda 2016 katika enzi ya Wayne Rooney.
Hiki kikiwa kichapo kizito zaidi kuwahi kupokezwa the Red Devils, Manchester United pia imepoteza mechi nyingi zaidi dhidi ya Liverpool kuliko mpinzani mwengine yeyote yule katika historia yao.

Tom Lutali is a seasoned scribe based in Lugari Sub-County in Kakamega County who writes human interest stories and sports for WKT.