
Ukurasa wa mbele wa Taifa Leo/Hisani
Taifa Leo
Gazeti hili linaripoti kuwa mbunge wa zamani wa Bonchari, Parvel Oimeke, amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu gerezani baada ya kupatokana na hatia ya kula hongo ya Sh 200,000 kutoka kwa mwanabiashara aliyekuwa akitafuta leseni ya kufungua kituo cha mafuta.
Mbunge huyo wa zamani alipokea pesa hizo kutoka kwa Wycliffe Oyoo.
Oimeke alikabidhiwa kifungo hicho na hakimu mwandamizi wa mahakama ya kesi za ufisadi ya Milimani Peter Ooko.
Daily Nation
Gazeti hili linaripoti kuhusu namna wanasiasa walipanga uvamizi katika shamba la familia ya Kenyatta.
Imeibuka kwamba polisi walifahamu njama ya uvamizi huo katika shamba hilo lililoko eneo la Kamakis kwenye Barabara ya pembeni ya Eastern Bypass, Nairobi, lakini hawakufanya chochote.
Udadisi wa Daily Nation umetambua kuwa njama hiyo ilipikwa siku ya Ijumaa na kuimarishwa vilivyo Jumapili.
Wabunge wawili, gavana wa zamani na mwanamziki maarufu wa Kiambu ni miongoni mwa waliochangia pakubwa katika kuwakusanya wahuni Ijumaa iliyopita katika kutekeleza uvamizi huo wa Jumatatu.
Vijana hao waliajiriwa kutoka kaunti za Kiambu na Nairobi, wakisafirishwa kutoka maeneo ya Ruiri, Githurai 45, Gatundu Kusini, Ruai, Kayole na Mathare mtawalia.
Duru zinadokeza kwamba vijana hao walilipwa Sh3,000 kila mmoja na kupewa mapanga na ‘power saw’ iliyotumika kukata miti katika shamba la Kenyatta.
Kulingana na chanzo hicho, taarifa za ujasusi zilitolewa mapema katika idara husika za usalama lakini hakuna maagizo yoyote yaliyotolewa.


Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.