Magazeti ya Ijumaa Machi 31 yanaangazia maandamano ya kiongozi wa Azimio Raila Odinga yaliyogeuka makabiliano kati ya wafuasi wake na polisi.
Aidha, kuna taarifa pia kuhusu ajali iliyohusisha basi la chuo kikuu cha Pwani katika eneo la Kayole Naivasha.
The Standard
Gazeti hili limeripoti kuhusu ajali ya basi la Chuo Kikuu cha Pwani ambalo lilihusika katika ajali eneo la Kayole Naivasha.
Watu 16, na sasa imefika 17, walifariki dunia huku wengine 50 wakibaki na majeraha mabaya na wanapokea matibabu katika hospitali.
Mkuu wa polisi Naivasha, Samuel Waweru, alisema ajali hiyo ilisababishwa na kufeli kwa breki za basi, hali iliyofanya matatu ya abiria 14 kugongwa na basi hilo.
Mwanafunzi kwa jina Brian Safari alisimulia jinsi aliponea ajali hiyo baada ya kuamua kuahirisha kusafiri alipougua.
Collins Oluyali is a popular columnist who reviews the Kenyan dailies every morning in the Magazetini section, giving it a political angle with facts weaved in rich Kiswahili. Collo is also a strategist in the WKT team.