Mgazetini: Ruto na Raila walegeza kamba
Ukurasa wa mbele wa The Star/Hisani

Mgazetini: Ruto na Raila walegeza kamba

Magazeti ya Jumatatu, Aprili 3, yameangazia kwa upana hatua ya rais William Ruto na hasimu wake kisiasa Raila Odinga kulegeza misimamo yao mikali na kukumbatia mazungumzo.

Taifa Leo

Gazeti hili linawatahadharisha Wakenya kuwa waangalifu baada ya wataalam wa afya kugundua aina mpya ya magonjwa ya zinaa nchini. Wataalam wa Taasisi ya Utafiti wa Matibabu nchini (KEMRI), wanasema kuwa magonjwa hayo yana uhusiano wa karibu na ugonjwa wa kisonono na hayajawahi kuonekana humu nchini mbeleni.

Wanawake wote 424 wenye umri wa kuanzia miaka 15 na kuendelea walioshiriki katika utafiti huo uliofanywa katika hospitali mbili tofauti walionyesha dalili za maradhi ya kisonono na chlamydia.

Wanawake hao walilalamika kuhusu kuwashwa, uchungu na kuvimba kwenye sehemu ya siri.

Vile vile walilalamikia harufu mbaya, kutoka uchafu, kuwashwa wakati wa haja ndogo, kuvuja damu kwa njia isiyokuwa ya kawaida na uchungu kwenye sehemu ya chini ya mgongo.

Share this article
Leave a Comment

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *