
Bruno Saltor/Courtesy
Baada ya kocha raia Mwingereza Graham Potter, 47, kuachishwa kazi, nafasi yake imechukuliwa na kocha wake msaidizi Bruno Saltor.
Bruno ni raia wa Uhispania ambaye alikuwa mchezaji wa Brighton kisha alipostaafu akajumuishwa kwenye benchi la ufundi la kocha Graham Potter na alikuja sambamba na Potter ndani ya Chelsea akiwa kama kocha msaidizi.
Bruno atabaki na Chelsea kama kocha wa muda mpaka pale nafasi hiyo itakapopatiwa kocha mwingine. Umri wake ni miaka 42.
Ataiongoza Wanasamati hao katika mechi kumi ambazo zimesalia katika ligi kuu nchini Uingereza.
Mechi yake ya kwanza kama mkufunzi huyo ni dhidi ya wekundu wa Anfield hapo kesho katika kuwania ligi kuu nchini Uingereza.
Chelsea walipoteza mechi yao Jumamosi dhidi ya Aston Villa 2-0 ugani Stamford Bridge mbele ya mashabiki wao.
Mechi yake ya pili ni dhidi ya Real Madrid juma lijalo katika Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya.
Raia huyo Mhispania amekuwa ligendari wa klabu ya Brighton na alijiunga na klabu hiyo mwaka wa 2012 amechezea vijana hao mechi 235 na kustaafu mwaka wa 2019 .

Thanks for choosing WKT. Advertise with us for affordable offers.